Mjomba wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameondolewa
madarakani. Taarifa hizo zimeripotiwa na shirika la habari la Yonhap, likinukuu
duru za kijasusi za Korea Kusini. Jang Song Thaek, mume wa shangazi wa
Kim, Kim Kyong Hui, alikuwa makamu mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya
Ulinzi na alikuwa akionekana kama kiongozi wa pili mwenye ushawishi
mkubwa nchini humo. Kim amekuwa madarakani tangu baba yake, Kim Jong
Il alipofariki mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment