Shambulio la anga lililofanywa na ndege isiyo na rubani ya kikosi cha Jumuiya
ya Kujihami ya NATO, limemuuwa kamanda wa kundi la Taliban katika eneo
la kaskazini-mashariki mwa Afghanistan. Afisa wa polisi, Ahmad Farid katika
mkoa wa Kunar karibu na mpaka wa Pakistan, amemtaja kamanda huyo kuwa
ni Hajji Attaullah. Vikosi vya kimataifa vinavyoongozwa na NATO,
vimethibitisha kuhusu shambulio hilo. Shambulio hilo limefanyika wakati
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO wanakutana leo mjini Brussels ambapo
pamoja na mambo mengine wanatarajia kuishinikiza Afghanistan kukubali
masharti ya kuendelea kwa shughuli za kikosi cha NATO baada ya jumuiya
hiyo kuondoka mwaka ujao, huku wakishauriana kuhusu mustakabali wa nchi
hiyo kufuatia operesheni kubwa ya kijeshi ambayo bado haijaanza.
No comments:
Post a Comment